3 Februari 2026 - 22:14
Sala na Ibada za Usiku wa Nusu ya Sha'bani (15 Sha'bani)

Tukiwafahamu wanadamu vizuri, tutagundua kuwa wengi waliotuzunguka walitukosea kwa ujinga, si kwa uadui. Hivyo basi, katika usiku huu mtukufu, tusameheane, tusafishe nyoyo zetu, na tumrudia Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Usiku wa tarehe 15 Sha‘bani ni miongoni mwa nyakati tukufu katika Uislamu. Ni usiku unaofuatia Lailatul-Qadr kwa ubora na fadhila zake. Katika usiku huu, Mtume Muhammad (saww) alikuwa akijitahidi sana katika ibada. Ni fursa adhimu kwa Muislamu kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu na ikhlasi.
Jitahidi, kadiri ya uwezo wako, kufanya ibada zifuatazo:

Ibada Zinazopendekezwa
Kuoga kwa nia ya Sunna ya usiku wa 15 Sha‘bani.

Kuswali rakaa 6, kila rakaa usome:
Al-Fatiha ×1
Yasin ×1
Al-Mulk ×1
Al-Ikhlas ×1
Kuswali Sala ya Ja‘far at-Tayyar.
Kusoma Qur-ani, angalau Juzuu 1–3.
Kufanya istighfari kwa wingi.
Kuswali Sala ya Usiku (Tahajjud) rakaa 11.


Fadhila Zake:
Miongoni mwa faida za ibada za usiku huu ni:
Kufunguliwa milango ya riziki.
Kuepushwa na mabalaa.
Kusamehewa madhambi.
Kuimarika kwa uhusiano wa mja na Mola wake.

Nasaha ya Maisha
Jitahidi katika maisha yako usikose kutafakari, kwani gharama ya kutozingatia ni kufeli na kuishi gizani. Mwenyezi Mungu amewaahidi Waumini Pepo ambayo upana wake ni sawa na mbingu saba na ardhi saba. Basi, kwa nini tuyastaajabie malipo ya ibada hizi?
Tukiwafahamu wanadamu vizuri, tutagundua kuwa wengi waliotuzunguka walitukosea kwa ujinga, si kwa uadui. Hivyo basi, katika usiku huu mtukufu, tusameheane, tusafishe nyoyo zetu, na tumrudia Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha